Shida Kwisha ana kisa, “Mrembo alinijulisha kuhusu mradi wa kuwekeza. Bila kuuliza maswali mengi niliingia. Nami niliwaambia watu wengi lakini ni wachache sana walionisikiliza. ‘Mtu hana kitu, ni uwekezaji gani atakwambia na umsikilize?’ watu walinichekelea.”
Wale watu wa zamani walikuwa watu wa kawaida. Walikuwa maskini wakabadilika kiasi cha kuwa matajiri si wa kutajika tu bali wa kutisha. Walipataje utajiri? Swali hilo lilikuwa kero kwao kwa kuwa walitaka wao wawe matajiri peke yao. Kiini cha utajiri kilikuwa siri kali. Siri kali hiyo ndiyo aliyoipata mtu aliyetambua umaskini si kizalia. Akaitoa hiyo siri kali ya siri kali tano kwa watu ili kila mtu aweze kuwa tajiri. Siri kali ilikuwa, ni na itakuwa dawa ya mabadiliko. Ukiipata na uitumie utatajirika. Ukiipata lakini usiitumie utabaki maskini vivyo hivyo.