Kwa sababu ya woga watu wanapoteza fursa nyingi sana maishani. Wengine wamepoteza nafasi ya kupata mchumba mzuri kwa sababu ya woga, wengine kwa woga siku ya interview wakakosa kazi na bado wengine fursa za biashara zikawapita. Lakini Neno la Mungu liko wazi kwamba huna haja ya kuogopa yeyote wala chochote ila Mungu Mwenyezi. Katika kitabu hiki, Biblia Inasema Usiogope, mistari mbalimbali katika Maandiko Matakatifu inachambuliwa kumpitisha msomaji kuanzia kuona kwamba woga ni dhambi hadi namna za kuishinda hofu na kutembea jasiri kama impasavyo mtu mwenye imani.
Hiki ni kitabu cha mafundisho ya Biblia yanayomfaa kila mtu lakini zaidi yule aliyebanwa na changamoto za kimaisha zinazomfanya ajawe na hofu kwa sababu ya kutoona uchochoro wa kutokea. Soma kitabu hiki na hutabaki mdhaifu tena.